Zitto Kabwe Amtetea Samatta "Msimuingize Kwenye Haya Mambo Tafadhali"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Amtetea Samatta "Msimuingize Kwenye Haya Mambo Tafadhali"
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka na kumtetea mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania ambaye sasa anakipiga klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji , Mbwana Samatta kuwa ameshinda kwenda kumtembelea Tundu Lissu kutokana na ratiba yake kuwa ngumu.

Zitto Kabwe aliona aweke wazi hilo kufuatia baadhi ya watu kuanza kuhoji inakuaje mchezaji huyo yupo ameshinda japo kwenda kumtembelea na kumuona Mbunge Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini humo kufuatia kushambuliwa kwa risasi mwaka jana. Zitto Kabwe ndipo aliamua kuweka sawa kuwa mchezaji huyo kwa sasa ratiba yake ni ngumu lakini anaamini atakwenda wakati ukipatiakana.

"Mbwana ni mgonjwa pia. Hivi sasa yupo kwenye mazoezi chini ya ratiba ngumu Sana ili arudi hali yake ya kawaida. Mjue kuwa Mbwana ni profeshno hawezi kwenda kinyume na ratiba ya daktari kama huko kwetu. Msimwingize kwenye haya mambo tafadhali. Atamwona Lissu kwa wakati wake" aliandika Zitto Kabwe

Zitto Kabwe kwa sasa yupo nchini Ubelgiji ambapo alipata nafasi ya kumtembelea Mbunge Tundu Lissu anapopatiwa matibabu pia aliweza kumtembelea mchezaji huyo wa Genk

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si kila mmoja anawehuka kwa Tundu Lissu.
    Kwani alipokuwa Kenya wabongo wengi kiasi gani walikwenda.
    Wengine mna jamaa zenu huko huko Bongo wamelazwa na hamuwatembelei.
    Acheni kumfanya Lissu kuwa big issue.
    Watu hawaachi yao eti Tundu kalazwa tukamtembelee.
    Asiyetaka kumtembelea nani ana haki ya kumhoji?

    ReplyDelete
  2. Sioni umuhimu wowote kwa Samata kwenda kumuona Ĺissu.Huyo Lissu alimjulisha Samata kwamba atakuwa Ubelgiji? Thawabu gani atapata Samata akienda kumuona huyo Lissu ambaye hamuheshimu Rais wa nchi yake?

    ReplyDelete

Top Post Ad