Hatimaye Wastara Arejea Nchini Akitokea India kwa Matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Wastara Arejea Nchini Akitokea India kwa MatibabuMSANII wa Bongo Movie, Wastara Juma amerejea Tanzania leo Alhamisi, Machi 1, 2018 akitokea  India alikokuwa akitibiwa mguu na mgongo katika Hospitali ya Saifee, Mumbai.

Akifanya mahojiano LIVE na Global TV Online, Wastara amesema kwa sasa yuko ‘fiti’ baada ya kupata matibabu hospitalini na anaweza kusimama mwenyewe na kutembea tofauti kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa lazima atumie baiskeli ya walemavu (wheel chair).


“Nilivyofika nilipokelewa kama wagonjwa wengine, nikapata vipimo vya awali na kupewa kitanda, baadaye walikuja madaktari kwa nyakati tofauti ambao walinipima mguu, tumbo na mwingine mgongo. Walibaini maambukizi kwa ndani hivyo nilifanyiwa upasuaji kuuondoa.

“Madaktari waligundua nilikuwa na tatizo la kupungukiwa damu, uvimbe kwenye mguu uliokuwa umekatwa, pia niligundulika kuwa na uvimbe kwenye utumbo na sikuwa najua ambapo nilifanyiwa upasuaji. Hivyo vyote nilifanyiwa upasuaji na kupatiwa dawa.

“Mbali na hivyo nilibainika kuwa na mpasuko kwenye fuvu ‘fracture’ ambayo nimeambiwa nitarudi tena kutibiwa kwani inaweza kuniletea matatizo baadaye. Kwa sasa namshukuru Mungu licha ya kushonwa upya na kupewa mguu mpya, ninaendelea vizuri, mguu ninaufanyia mazoezi. Lakini kwa mgongo maumivu yanazidi kupungua polepole wakati nikifanya mazoezi,” alisema Wastara.

Aidha, Wastara amemshukuru tena Rais John Magufuli kwa kujitoa kwake kumsaidia kufanikisha matibabu yake;

“Namshukuru Rais Magufuli kwa kujitoa kwake, ndoto yangu ilikuwa siku moja nisimame niweze kufanya kazi zangu, na leo hii imewezekana. Kusimama kwangu kunawafanya watu wengi walioko nyuma yangu wanaonitegemea kufanikisha maisha yangu. Uzima huu nilikuwa nauhitaji kwa ajili ya kufanya kazi na hivi karibuni nitasimama,” alisema akielezea shukurani zake kwa rais.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad