Hivi Ndivyo Wastara Alivyokutana na Islaeli Mtoa Roho za Watu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hivi Ndivyo Wastara Alivyokutana na Islaeli Mtoa Roho za WatuMWANAMAMA wa Bongo Movies aliyepitia masahibu mengi ya kimaisha, Wastara Juma amesema kuwa kutokana na mateso na magonjwa yanayomkabili, ameshamuona Malaika Israel Mtoa Roho mara nyingi mno, lakini kwa sababu Mungu bado anampenda, anaendelea kudunda kwa neema zake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda mara baada ya kurejea kutoka nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu, Wastara alisema kuwa, alikuwa akikiona kifo mara nyingi mno, lakini anaamini Mungu anampenda ndiyo maana amemwacha salama hadi leo.

“Nimeshamuona Israel Mtoa Roho mara nyingi sana, lakini kwa sababu Mungu ananipenda, bado ninapumua. Ninaamini Mungu atanipa uhai mrefu kutokana na majaribu niliyopitia,” alisema Wastara ambaye alikatika mguu kabla ya kufiwa na mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ n asana anakabiliwa na magonjwa mbalimbali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad