Kenyatta, Odinga Kimeeleweka! Waandaa Kufanya Ziara ya Kuzunguka Nchi Nzima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kenyatta, Odinga Kimeeleweka! Waandaa  Kufanya Ziara ya Kuzunguka Nchi Nzima
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na  hasimu wake ambaye ni kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga wamepanga kufanya ziara ya nchi nzima kuhamasisha amani, mshikamano na umoja.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia maeneo ambayo vyama vya upinzani nchini humo vina nguvu zaidi na kuendelea maeneo mengine.

Gazeti hilo limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia jimbo la Nyanza ingawaje tarehe rasmi ya ziara hiyo bado haijatangazwa.

Wakati hayo yakijiri, viongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya leo Jumatatu wanatarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu mustakabari na muelekeo wa umoja huo.

Wiki iliyopita Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga alikutana na Rais Uhuru Kenyatta kwenye Ikulu ya nchi hiyo ambapo kwa pamoja walikubaliana kujenga nchi na kuweka mbali tofauti zao za kisiasa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya sasa nyie mnaopenda maandamano kwa kufuata mkumbo mtaweka wapi sura zenu......na wale walo uwawa-vepe? Ama kweli, siasa ni mchezo mchafu, hauna rafiki wakudumu wala adui wakudumu......wanapogombana shika-jembe ukalime..........TAFAKARI

    ReplyDelete

Top Post Ad