Mafuriko Yasababisha Ofisi za Mwendokasi Kuhamishwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mafuriko Yasababisha Ofisi za Mwendokasi Kuhamishwa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Udart) umeamua kuhamisha ofisi zake kwa muda ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa amesema wamehamisha ofisi hizo ili shughuli zinazofanywa na mradi huo zisiweze kutetereka kutokana na mvua zinazoendelea.

"Maji yalianza kujaa saa nane usiku, tulianza kuhamisha magari yetu yote na kuyapeleka katika vituo vikubwa vya mabasi yetu, licha ya mabasi pia tumehamisha vitu vingi vya ofisi kwa sasa hatutaitumia kwa muda," amesema Bugaywa.

Amesema wameamua kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, kutokana na maji kujaa eneo la jangwani na hivyo barabara hiyo ilifungwa tangu saa kumi alfajiri na imefunguliwa saa tatu asubuhi baada ya trafiki kujiridhisha kwamba inafaa kupitika.

Imewekwa wazi kuwa ofisi zilizopo eneo la Jangwani kwa sasa hazitatumika na mabasi yote yaendayo haraka yatalazwa katika vituo vikuu vya mabasi hayo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad