Masogange Amelazwa Hawezi Kutembea, Ashindwa Kufika Maakamani Kusikiliza Hukumu Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Masogange Amelazwa Hawezi Kutembea, Ashindwa Kufika Maakamani Kusikiliza Hukumu Yake
Leo March 2018  Video Queen, Agnes Gerald maarufu ‘Masogange’ ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza HUKUMU ya kesi yake ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam kwa sababu amelazwa hospitalini amewekewa Dripu na hawezi kutembea.

Hayo yameelezwa na Mdhamini wa Masogange, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa serikali, Adolf Mkini kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya hukumu.

Mdhamini wa Masogange, alisimama na kumueleza Hakimu Mashauri kuwa Masogange ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anaumwa.

“Masogange anaumwa yupo hospital amelezwa na kuwekewa Drip, pia hawezi hata kutembea,” -mdhamini.

Katika kesi hiyo, Masogange anawakilishwa na Wakili Ruben Simwanzi ambaye ameeleza kuwa mteja wake anaumwa.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha hukumu hadi April 3,2018.

Awali katika ushahidi wake Masogange alidai kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya, hivyo anaiomba Mahakama imuachie huru kwa sababu hana kosa.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad