Mwenyekiti UVCCM Amvaa Waziri Shonza "Mnawafungia Kina Roma, Daimond Mtaimba Nyie"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti UVCCM Amvaa Waziri Shonza "Mnawafungia Kina Roma, Daimond Mtaimba Nyie"
Kufuatia sakata la kufungiwa kwa baadhi ya wasanii na nyimbo zao, akiwemo Roma Mkatoliki, Diamond Platnumz, Snura na wengine, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James, amekerwa na maamuzi hayo yaliyofanywa na Basata na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kupitia kwa Naibu wake, Juliana Shonza.



Akizungumza jana Mjini Dodoma, Kheri James alieleza masikitiko yake na kusema kuwa wizara hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya wasanii ambao wengi wao ni vijana wanaojitafutia kipato kupitia tasnia hiyo.



“Mmemfungia Roma, mmemfungia Diamond na wengine, kila anaenyanyuka mamkata mguu, hivi mnavyowafungia mtaimba nyie?



“Kama wizara itendelea na tabia hiyo ya kuwafungia wasanii, na wao ndio viongozi wa sanaa je watamsimamia nani wakishawafungia wote?” alihoji Kheri.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kakutuma nani mshikaji?
    Kwani CCM inapowatimua viongozi ni kwa lengo gani?
    Ukiacha Roma na Daimondi, kwani tz haina vijana wengine wNaotumbuiza vzuri tu kwa kufuata maadili ya nchi na sheria zilizowekwa?
    Kwani hao uliowataja ndio hatimiliki ya muziki wote wa bongo flava?
    Mbona kumbe mheshimiwa nawe hufanani na wadhiwa uliopewa?
    Vp unashindwa kupambanua issue nyepesi tu kama hii?
    Nikukumbushe: Kule nchini Italia kuna timu zilishushwa daraja. Kule Scotland nako ni hivo hivo. Zote sababu ni kuvunja sheria za futiboli nchini kwao.
    Na halikusababisha kandanda kumalizika.
    Nikukumbushe: Mrema alikuwa waziri wa CCM. Seif Sharrif alikuwa waziri kiongozi wa serikali ya CCM.
    Sumaye alikuwa waziri mkuu mstaafu wa CCM. Lowassa alikuwa ndani ya NEC ya CCM.
    Kimbau alikuwa kiongozi CCM.
    Niendelee?
    Nadhani wanatosha.
    Je hawa wote wako wapi sasa?
    Je CCM mwimbaji nani sasa?
    Mheshimiwa James jiangalie usije ukatumbuliwa!!
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete

Top Post Ad