Rais Magufuli Ayaonya Maandamano ya Mange Kimambi "Ngoja Waandamane Wataniona"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Ayaonya Maandamano ya Mange Kimambi "Ngoja Waandamane Wataniona"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia suala la maandamano na kusema atashughulika na watu ambao wataandamana ili wakawasilimulie wale watu ambao wamewatuma.


Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 9, 2018  wakati akizindua tawi la benki ya CRDB Chato na kusema kuwa wapo watu ambao wanataka kuona amani ya nchi hii inavurugika jambo ambalo yeye hawezi kukubali kwa kuwa alihapa kulinda Katiba ya nchi.

"Wapo watu wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuwe barabarani tunaandamana, watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamana kule nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri mwanzo ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali" alisema Magufuli.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uko vizuri Mkuu Magufuli ila hao watanzania wachache wa hovyo wasikusumbue kabisa. Tayari umeshashinda vita ya uongozi wa kuliongoza Taifa katika misingi ya kiuajibikaji kinachotakiwa ni kudumishwa na kulindwa jitihada hizo. Hizi kelele za hao wanaotaka kufanya maandamano ni sawa na kelele za wasafiri ndani ya Treni haziwezi kusumbua kasi ya treni na kama dereva mahiri ongeza kasi tu itafika mahali watalala wenyewe wakiiacha treni ikiendelea na safri.

    ReplyDelete

Top Post Ad