RC Makonda Atangaza Vita na Wanaume Wasiotunza Watoto Wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RC Makonda Atangaza Vita na Wanaume Wasiotunza Watoto Wao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita na wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuwatelekeza kwa kuandaa jopo la Wanasheria watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume hao kuanzia Aprili 09 mwaka huu kwenye ofisi yake.


Taarifa hiyo imetolea na ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo imesema kwamba kitendo cha Wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imepelekea pia baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu kulelewa na wazee na kusababisha mzigo kwa familia.

Aidha RC Makonda amesema kuwa wataangalia pia utaratibu wa kufanya marekebisho sheria ya gharama za matunzo ya mtoto kwakuwa ni ndogo na haiendani na hali ya sasa.

RC Makonda amesema lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Hata hivyo Makonda amesema katika zoezi hilo lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Pamoja na hayo Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesena kwamba  ameamua kutoa muda wa mwezi mmoja ili kama kuna baba kwenye huu Mkoa huo anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa matunzo kwakuwa itakapofika Aprili 09  atachukuliwa hatua kali za kisheria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo sawa Makonda katika utatisha sana kiutendaji. kwani hata ukichunguza chanzo cha kupata ujauzito kwa akina mama mara nyingi wanaume ndio huwa wa mwanzo kuhamasisha tendo la ndoa. Lakini mtoto akizaliwa tunajifanya kama hatukuhusika na kuja kwa kijacho. Naomba Mungu, suala hili lichukuliwe serious sio kwa Daresalam tu bali Tanzania nzima. Ikiwezekana hata ikiwepo sheria ya kumpeleka mtu jela kwa kushindwa kutimiza majukumu yake juu ya malezi kwa mtoto na kumuachia mwanamke akiteseka na watoto peke yake wakati yeye akila Bata.

    ReplyDelete

Top Post Ad