Timu ya Simba Yapata Pigo Mchezaji Wao Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Timu ya Simba Yapata Pigo Mchezaji Wao Afariki DuniaMchezaji wa Zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam.


Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.

"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki", amesema Manara.



                                        Marehemu Arthur Mambeta  enzi za uhai wake.

Uongozi wa EATV kwa pamoja unawapa pole wadau wa soka nchini, familia ya marehemu na klabu ya Simba kwa kuondokewa na mtu muhimu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad