Watu 108 Waokolewa Katika Ajali ya Boti DRC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu 108 Waokolewa Katika Ajali ya Boti DRCIdadi kubwa ya watu inasadikiwa kupotea baada ya boti kuzama nchini DRC,huku jitihada za kuwaokoa zikiendelea. Mpaka sasa taarifa juu ya idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani ya boti hiyo hazijasemwa, huku mbunge wa jimbo lilipotokea ajali hiyo Didas Pembe alitangaza kuwa inawezekana ni zaidi ya watu 500 ndio wamepotea.

Licha ya kutangazwa kutokea kwa ajali ya boti hiyo usiku wa Jumatatu hadi Jumamne nchini DRC jimboni Mayi -ndombe magharibi mwa mji mkuu wa Kinshasa,mbunge wa jimbo hilo ambae alitangaza taarifa hiyo alisema idadi aliyoitangaza awali hazikuwa za uhakika kwa kuwa taarifa alizopata hazikuwa za kweli. Lakini mara baada ya mbunge huyo kufika katika eneo la tukio alisema boti hiyo ilikuwa na abiria 121 na watu 108 wameokolewa huku watu 12 ndio wamepotea mpaka sasa na kifo cha mtoto moja wa miaka tano.

Aidha kuna ripoti kutoka kanisa la jimbo hilo wamesema kwamba watu kumi na tano ndio waliofariki ,Huku wahudumu wa afya wamethibitisha kupokea miili ishirini na tano na wakisema boti hiyo ilikwa na abiria wengi waliokuwa wakisafiri mjini Kinshasa.

Leo bado inasubiriwa ripoti kutoka msalaba mwekundu maana bado idadi kamili haijatajwa na imekuwa inatofautiana sana.

Ajali za boti zimekuwa zikiripotiwa karibu kila mwaka nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo kufuatana na ubovu wa boti na mashua na huku wakisafiri bila mavazi ya kujiokolea katika maji.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad