Yanga Kumuondoa Simba Kileleni?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Kumuondoa Simba Kileleni?
Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imewataka mashabiki zake na wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi leo uwanja wa Taifa ili waweze kushuhudia jinsi wanavyochukua alama zao tatu dhidi ya Stand United.


Hayo yameelezwa na mlinzi wa nyuma upande wa kulia wa wanajangwani Juma Abdul muda mchache alipomaliza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuelekea mchezo wao wa Ligi kuu unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

"Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumeweza kumaliza salama mazoezi kwa siku ya leo ila kikubwa tunachoweza kusema tunawaomba mashabiki wa Yanga SC kesho waweze kujitokeza kwa wingi. Wao wanaojitokeza kwa wingi sisi ndio inatupa hamasa na kuweza kufanikisha katika mchezo wetu dhidi ya Stand United", amesema Juma Abdul.

Pamoja na hayo, Abdul ameendelea kusema "ubingwa unawezekana hakuna kukata tamaa, pointi tatu leo kama kawaida".

Timu ya Yanga inashuka dimbani ikiwa imeshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu kwa alama 43, Azam FC imeshika nafasi ya pili kwa pointi 44 baada ya kufanikiwa kumchapa Mbao FC siku ya jana kwa mabao 2-1 huku Simba SC akiwa ameshikilia usukani mpaka dakika hii kwa alama 46 ambapo leo hii kuna hati hati ya kunyanganywa kijiti hicho na Yanga SC endapo watafanikiwa kuwaburuza Stand United.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad