Maandalizi ya Harusi ya Alikiba Kufulu Tupu ...... Mapambo tu Zaidi ya Milioni 40

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maandalizi ya Harusi ya Alikiba Kufulu Tupu ...... Mapambo tu Zaidi ya Milioni 40
Wakati zikiwa zimesalia saa chache kabla mwanamuziki Alikiba hajafunga ndoa jijini Mombasa, imebainika kuwa ametumia mamilioni katika maandalizi ya sherehe hiyo.

Mwandishi wetu aliyepo Mombasa, Mohammed Ahmed anaripoti kuwa mapambo katika ukumbi utakaofanyika sherehe hiyo yamegharimu Sh2 milioni za Kenya ambazo ni wastani wa Sh40 milioni za Tanzania.

Mpambaji wa ukumbi wa Diamond Jubilee unaochukua watu 1,500 katika jiji hilo ambaye mwandishi wetu alimkuta akiendelea na kazi,  anasema amelipwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni kikubwa kulingana na aina ya mapambo waliochagua maharusi.

Alikiba anayetamba na wimbo Seduce Me anatarajia kufunga ndoa kesho na mrembo Amina ambaye anatokea Mtaa wa Kongowea katika jiji hilo.

Inaelezwa kuwa familia ya binti huyo ina uhusiano wa karibu na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ni rafiki wa Alikiba.

Inaaminika kuwa Joho ndio amesaidia kwa kiasi kikubwa kumuunganisha Kiba na familia ya Amina, ambapo safari zake za mara kwa mara mjini Mombasa, hazikuwa kwa shughuli za kimuziki tu bali ni kuwa karibu na mkewe huyo mtarajiwa.

Harusi hiyo inatarajiwa kurushwa mubashara kwenye runinga ya Azam kuanzia Mombasa ambako Joho na vigogo wengine wa Muungano wa NASA wanatarajiwa kuhudhuria huku sherehe ya hapa nchini, Tanzania Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete anatajwa kuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad