Makonda Kupima Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba kwa Lazima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Kupima Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba kwa Lazima
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda, anatarajia kuanza mkakati maalum wa kupima tezi dume kwa lazima nyumba kwa nyumba mkoani Dar es salaam.


Taarifa hiyo imetolewa leo na mwenyewe Paul Makonda alipokuwa akizindua warsha ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana, ikihusisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa, na kusema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba, lakini hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo.

“Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu, kuhakikisha hii kasi ya vifo vya kina baba kwa tatizo la tezi dume inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu”, amesema Paul Makonda.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Dar es salaam amewataka viongozi wote wa serikali za mitaa na viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wafike kwenye vituo vya afya vinavyotoa chanjo hiyo kwa wingi kupata chanjo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Amuanze Lemutuz na kibamia chake, than ajipime mwenyewe ajue kwa nn Manii yake yake hayatengenezi watoto. mpka mkewe apandikizwe shahawa za mtu asomjua?

    ReplyDelete
  2. Wazo la kupima ni zuri kabisa, ila upimaji utanguliwe na campaign maalum ya uhamasishaji na advocacy. Ila iwe mwiko kulazimisha upimaji. Consent ya client ni muhimu na ni moja ya maadili na nidhamu ktk fani nyingi zinazo deal na afya za binadamu

    ReplyDelete

Top Post Ad