"Baba yangu Alipigana vita ya Kagera" - Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amebainisha kuwa baba yake ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao wamepigana vita nyingi kwaajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya kagera mwaka 1978.


Mh. Paul Makonda amesema hayo leo Mei 17, 2018 wakati wa alipokuwa anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi

“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania” amesema Makonda

Makonda aliongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.

Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad