AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Belle 9 alipata shavu la kusainiwa na label ya ‘Vitamin Music’ ambayo ilimuhamisha kutoka Morogoro na kumleta Dar kwa ajili ya kufanya Muziki lakini baada ya kuoa Belle 9 alipotea kidogo.
Baadae zilizuka stori kuwa Belle 9 ameamua kurudi nyumbani Morogoro kutokana na kukosa shoo na kufulia hapa Dar kiasi ya kwamba ana kosa hata pesa ya kulipia kodi ya nyumba.
Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Belle 9 amekana tetesi hizo za kufulia na kusema hajahama Dar bado yupo mjini:
"Dah Hapana muda mrefu sijafika Morogoro mi Nipo Dar, hizo ni rumors tu zinazosambazwa na watu Lakini pia naona wanasema hivyo kwa sababu sionekani Kwenye maeneo ya starehe mengi."
Belle 9 amerudi upya na kazi yake mpya aliyotoa siku chache zilizopita inayokwenda kwa jina la ‘Dada’.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK