Mtoto wa miaka mitatu aliwa na chui Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kutoka nchini Uganda, Maafisa wa Wanyamapori wanaendelea kumsaka chui aliyemshambulia na kumla mtoto wa miaka mitatu pamoja na mwangalizi wa Hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth.

Tukio hilo linaelezwa kutokea Ijumaa ya wiki iliyopita ambapo mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Elisha Nabugyere alimfuata mlezi wake nje ya nyumba yao ambayo haikuwa na uzio na ndipo chui huyo alipomuona na kumshambulia.

Msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi nchini Uganda Bashir Hangi ameeleza kuwa mlezi huyo hakujua kuwa mtoto alimfuata nje, lakini alisikia kelele za mtoto huyo kulia na alivyotoka nje chui huyo alitokomea hifadhini na mtoto huyo.

Hangi amesema kwamba siku mbili mbele walipata fuvu la kichwa tu la mtoto huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad