Mwanasayansi Kuuliwa na Sindano ya Sumu Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall,  kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.


Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.

Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.

Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.

David Goodall

Katika mahojiano Goodall amenukuliwa akisema "Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. "Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?

Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10 iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama kifo kingemchukua katika miaka hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad