Nyumba ya Joti Yabomolewa Afunguka Kisa Kizima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nyumba ya Joti Yabomolewa Afunguka Kisa Kizima
Hapo jana May 03, 2018 Mchekeshaji Lucas Mhavile ‘Joti’ aligonga vichwa vya habari mara baada ya kuwepo taarifa zilizodai kuwa nyumba yake iliyopo Kibada, Kigamboni imevunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara, sasa Joti ameeleza kilichotokea.

Akiongea na Clouds FM amesema si kweli kwamba nyumba yake imevunja bali ni ukuta ndio umewekwa alama ya X ila amekiri kuwepo kwa zoezi hilo.

‘’Wanapanua barabara huku kwetu, lakini huo upanuzi wa barabara haujahusiana na ubomoaji wa nyumba, wengi wanajua nyumba yangu ndio inabomolewa lakini sivyo, kinachobomolewa ni ukuta tu,’’ amesema Joti.

Kwa mujibu wa Afisa Manispaa ya Kigamboni, Davidi Langa wakazi zaidi ya 100 wa Kibada na Kisarawe wilayani Kigamboni nyumba zao zimewekea alama ya X na kutakiwa kubomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara.

Chanzo cha tatizo ni Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi iliyopima maeneo hayo, Tanroad walikuwa bado hawajaweka alama zao za barabarani na viwanja hivyo ni vya muda mrefu, hivyo wamekuja kuweka wakati vimeshaendelezwa, hata hivyo Mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa ameingilia kati suala hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad