Jay Z na Mkewe Beyonce Waachia Albamu ya Pamoja Wamtaja Trump

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jay Z na Mkewe Beyonce Waachia Albamu ya Pamoja Wamtaja Trump
Kumekuwepo na tetesi kwa muda mrefu lakini hatimaye nyota wa muziki - Beyonce na mumewe Jay-Z - wametoa albamu yao ya pamoja.

Albamu hiyo imepewa jina Everything is Love (Kila Kitu ni Mapenzi).

Albam hiyo inapatikana katika huduma ya kusikiliza na kununua nyimbo mtandaoni inayomilikiwa na Jay-Z kwa jina Tidal.

Beyonce alitoa tangazo la kutolewa kwa albamu hiyo akiwa kwenye jukwaa London na wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kujitokeza kuwatazama wakati wa tamasha yao ya kuizuru dunia.

Alisema: "Kwa sababu twawapenda sana, tuna kitu cha kipekee sana kwa ajili yenu."

Beyonce na Jay-Z katika video yao mpya ya muziki, nyuma yao ni picha ya Mona Lisa
Video ilichezwa kwenye skrini na mwishowe kukatokea ujumbe kwamba 'ALBAMU IMETOKA SASA'.

Video ya muziki ya dakika sita ilitolewa punde baadaye, ambayo iliandaliwa katika makumbusho maarufu duniani ya Louvre mjini Paris.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad