Kauli ya Chadema Baada ya Lembeli Kurudi CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kauli ya Chadema Baada ya Lembeli Kurudi CCM
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Afisa Habari wake Bwana Tumaini Makene kimetoa shukurani na kumtakia kila la heri kwa aliyekuwa mwanachama wao James Lembeli baada ya kutangaza kujiunga tena na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Akiongea na www.eatv.tv leo Juni 14, 2018 Afisa habari huyo amesema kwamba wanamshukuru Mbunge huyo wa zamani wa Kahama, katika kipindi alichokuwepo katika chama chao na kuongeza kuwa hawezi kuelezea sababu zilizopelekea Mbunge huyo kurudi tena CCM.

“Tunamshukuru kwa muda wake aliokuwepo CHADEMA kuanzia mwaka 2015, namimi ndiyo chama kiliniagiza kwenda kumuandalia mkutano na waandishi wa habari kwamba anahama CCM na akazungumza sababu za msingi sana kwanini anahamia CHADEMA kuunga mkono mabadiriko, kwahiyo tunamshukuru kwa muda wake katika kuunga mkono mabadiriko, tunamtakia kila la heri huko ambapo ameamua kurudi” amesema Makene.

Afisa habari huyo ameongeza kuwa, chama hicho bado kitaendelea kusonga mbele kupambana ili kuleta mabadiriko nchini, amesema “Gurudumu la mabadiriko linasonga mbele, halisimami ndiyo kwanza linashika kasi kuleta mabadiriko ya kweli ndani ya nchi hii tunamtakia kila heri kwa kuamua kurudi nyuma”.

Julai 21, 2015 akiwa Mbunge wa Kahama kupitia CCM, James Lembeli alitangaza kujiunga na CHADEMA, kabla ya jana Juni 13, 2018 kurudi tena chama chake cha awali CCM na kusema kuwa kitendo cha kuhamia CHADEMA kilimhuzunisha kwa kiasi kikubwa mama yake ambaye ni mwanachama wa CCM.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad