KIMENUKA..Baba Diamond na Baba Ommy Dimpoz Warushiana Maneno

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba mzazi wa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz,  Mzee Faraji Nyembo amemtolea povu Baba wa staa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma kutokana na tabia yake ya kumsema mwanaye vibaya.


Gazeti la Risasi Mchanganyiko  linaripoti kuwa Kwenye mahojiano waliyofanya na Baba Ommy Dimpoz alitoa taarifa ya mtoto wake kuendelea vizuri na kusisitiza hata kama mtoto wake hamsaidii kwa lolote maishani lakini hawezi kumsema vibaya kama Baba Diamond anavyofanyaga kwa mwanaye.

Unajua mimi ni mzazi wa tofauti sana, siwezi kumlalamikia au kumsemea mabaya mwanangu kwenye vyombo vya habari kama anavyofanya baba Diamond, ninachofanya huwa namuombea mwanangu awe na maisha mazuri maana nikimuombea mabaya anaweza kupoteza dira ya maisha yake nitakuwa nimefaidika na nini.

Namshauri baba Diamond awe anamuombea mwanaye mafanikio, aungane naye wawe kitu kimoja, afurahie mafanikio yake ipo siku Mungu atamrudisha kwake amsaidie na siyo kumzungumzia maneno ya kumlaani na kumlalamikia kila siku.

Aige mfano wangu maana mimi huwa simlazimishi mtoto anisaidie bali huwa napambana na hali yangu kwa kufanya kazi kwa bidii na ninampenda sana mwanangu Dimpoz na siwezi kumlaani au kumlaumu maana jina nililompa la Omary ni la baba yangu inakuwaje sasa nimlaani ni sawa na kumlaani baba yangu”.

Baada ya povu hilo gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond na kumuhoji kuhusu kile alichosema Baba Dimpoz na alimwaga povu hili:

Sitaki shobo, huyo baba Dimpoz simfahamu kama hana la kuongea anyamaze, amzungumzie mwanaye hata kama niliongea kuhusu Diamond si mtoto wangu yeye inamuhusu nini?”.

Kuhusu huyo Diamond sihitaji kuzungumza chochote kuhusu yeye wala watoto wangu maana hawana faida yoyote kwangu kwa sasa”.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad