Majambazi Wavamia Duka la Jumla Waua Mlinzi kwa Risasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majambazi Wavamia Duka la Jumla Waua Mlinzi kwa Risasi
Mkazi wa Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela jijini hapa, aliyetambulika kwa jina moja la Saytaa ameuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akijaribu kupambana na majambazi waliovamia maduka.

Akizungumzia tukio hilo, leo Juni 22, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Ilemela, Khadija Nyembo amesema tukio hilo limetokea jana Juni 21 saa sita na nusu usiku.

Amesema baada ya mlinzi huyo kusikia mlio wa bunduki alienda sehemu ya tukio kutoa msaada wa kuwadhibiti wahalifu hao ndipo alipouawa.

Majambazi hao wanaodhaniwa walikuwa na silaha za moto walivamia duka la jumla la vifaa vya ujenzi na duka la nguo lililokuwa pia lina huduma za kifedha na kupora fedha kisha kumuua mlinzi huyo.

Nyembo ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo amesema: “Watu waliposikia mlio wa bunduki hawakutoka lakini yeye alienda, katika kupambana nao bila kuchukua tahadhari wakampiga risasi.”

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugogwa, Alphonce Bundege amesema, licha ya mtaa wao kuwa na askari wa doria lakini siku ya tukio walichelewa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad