Mfahamu Mwanamke Anayeweza Kukutabiria Siku ya Kifo kwa Kunusa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ari Kala raia wa Australia mwenye miaka 24 amegeuka gumzo duniani baada ya kudai kuwa ana talanta ya kugundua watu wanaokaribia kufa kwa kunusa tu harufu zao lakini cha kushangaza ni kwamba talanta yake hiyo haimuwezeshi Ari kumsaidia mtu anayekaribia kufa aepukane na kifo.

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anasomea taaluma ya saikolojia anasema kuwa aligundua talanta yake hiyo alipokuwa na miaka 12 alipokuwa ameenda kumtembelea mjomba wake aliyekuwa amekaribia kufa na ndipo aliponusa harufu mbaya ya mtu anayekaribia kufa ambayo hakuna mtu mwingine aliyeweza kunusa harufu hiyo.

“Nilidhani ni harufu ya mabaki ya mwili wa mjomba kwa sababu ilikuwa harufu mbaya sana ambayo sijawahi kuinusa. Lakini hakuna mtu mwingine aliyeweza kuinusa harufu hiyo” alisema Ari.

Ari aliongeza kuwa baadae alikuja kugundua kuwa mara kwa mara ameweza kunusa kifo na kuna wakati mwingine anaona ni mzigo kuwa na talanta hiyo na huwa anatamani kuwaambia watu wanaotaka kufa kwamba wanakaribia kufa lakini baadae huacha kwa sababu hilo sio jukumu lake.

Kwa sasa Ari Kala anawafundisha wanawake wenye umri kati ya 25-45 wanaotoka kwenye jamii zinazoamini uchawi kutumia vizuri talanta na vipaji vyao katika kuisaidia jamii.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad