Niyonzima Aondolewa Kikosini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima amepumzika kucheza soka na sasa atakuwa akipata matibabu kuhakikisha anarejea vizuri dimbani na hatakuwa katika kikosi kitakachocheza michuano ya Kagame.


Niyonzima alirejea uwanjani baada ya kupata matibabu nchini India ambako alipata matibabu kabla ya kurejea nchini na kuanza mazoezi taratibu, aliumia wakati wa michuano ya SportPesa Super Cup ingawa mechi ya mwisho ya fainali hakucheza kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano.

Habari kutoka Simba zimeeleza, Niyonzima aliumia licha ya kwamba alikosa mechi ya mwisho kutokana na kadi, hivyo atalazimika kukosa michuano ya Kagame, ndiyo maana ni kati ya wachezaji watakaopumzishwa katika michuano ya Kagame.

Kiungo huyo Mnyarwanda amekuwa na wakati mgumu tokea ametua Simba kutokana na kuandamwa na majeraha.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad