AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Trump akizungumza baada ya kutia saini hati hiyo amesema ameridhika kabisa na mazungumzo na wameanzisha uhusiano mzuri kati yao.
"Ninadhani uhusiano kamili kati yetu na Korea Kaskazini utabadilika na kua tofauti na namna ilivyo kua awali na tumeweza kukuza uhusiano mzuri kuliko vile tulivyotarajia."
Akiulizwa ikiwa atamualika Kim Washington alijibu, Bila shaka.
Kim kwa upande wake amesema wamekubaliana kuacha nyuma yaliyopita na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano.
Kabla ya kutia saini Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza na kupeana mkono asubuhi katika hoteli ya Capella kwenye kisiwa cha mapumziko cha Sentosa, huko Singapore.
Baadae tena wakakutana ana kwa ana kwa karibu dakika 40, kabla ya kutoka na kukutana pamoja na wajumbe wao wa vyeo vya juu. Katika mkutano huo kulikuwepo mawaziri wa mambo ya nchi za nje na wakuu wa usalama wa taifa wa kila upande.
Walipomaliza mazungumzo hayo viongozi hao walikula chakula cha mchana wakiendelea na mazungumzo bila yakufahamika kile walichokua wanazungumza.
Miongoni mwa masuali muhimu ni namna ya kuangamiza kabisa silaha za nuklia za Korea kaskazini, kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani huko Korea Kusini, suala la wajapan walotekwa nyara, kuheshimiwa haki za binadam, Korea Kaskazini, kuondolewa vikwazo na ushirikiano wa baadae kati ya nchi hizi mbili.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK