Waziri wa Maji Kavunja Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Maji na Umwagiliaji (Eng) Isack Kamwele amemsimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi, Romanus Mwang'ingo kwa tuhuma za ubadhirifu na udanganyifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima maeneno ya Kimbiji na Mpera huko Kigamboni, Jijini Dar es salam.


Maamuzi hayo ya Waziri Kamwele yamekuja leo Jumatatu, Juni 18 baada ya serikali kupokea taarifa za kuwepo kwa udanganyifu katika mradi huo ambapo mbali na ubadhirifu uliogundulika pia upo udanganyifu wa idadi ya visima  vilivyokamilika kama ambavyo taarifa zilizowasilishwa wizarani  na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji miradi.


Aidha Taarifa ya Waziri Kamwele imesema kuwa kutokana na kuwa Mhandisi Mwang'ingo ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa mradi huo kwa niaba ya DAWASA na seerikali basi anatengua nafasi yae hiyo ili kupisha uchunguzi wa TAKUKURU.


Aidha Waziri amemteua Dkt. Sufian Masasa kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.


Pamoja na hayo Waziri Kamwele amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi huo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad