Ajali: Hiace Yawaka Moto Barabarani Mbeya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ajali Nyingine Yatokea Mbeya
Ajali nyingine yatokea mbeya ambapo gari aina ya Toyota Hiace iliwaka moto ikiwa barabarani, ndani yake kulikua na Konda na Dereva ambao wote wamenusurika.

Mkoa wa Mbeya umekumbwa na ajali mfululizo hivi karibuni mpaka kupelekea Viongozi wa dini na Wazee wa kimila kufanya maombi kulikemea zimwi hilo ambapo ikiwa ni siku chache baada ya maombi hayo, ajali nyingine zimetokea usiku wa kuamkia leo.

Usiku wa kuamkia leo gari aina ya Land Cruiser limeigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu watatu kwenye eneo la Kadege usiku wa kuamkia leo ambapo usiku huohuo gari aina ya Toyota Hiace imewaka moto ikiwa barabarani katika eneo la Mbembela ambapo Dereva na Kondakta waliokuwemo ndani yake wamenusurika.



Ikumbukwe kuwa baada ya ajali iliyotokea katika mteremko wa Mbalizi, Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alitangaza kuyavunja mabaraza ya Usalama Barabarani ya Mikoa na Wilaya zote nchini.

Waziri huyo pia alimshusha cheo aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) wa Jiji la Mbeya, Leopold Fungu hadi kubaki na nyota 3 ambapo baada ya hatua hizo, ajali nyingine ilitokea katika mteremko wa Igawalo na kuua watu watano na kujeruhi mmoja.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad