Ed Sheeran yamemkuta! Adaiwa Bilioni 225 Baada ya Kukopi Wimbo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ed Sheeran yamemkuta! Adaiwa Bilioni 225 Baada ya Kukopi Wimbo
STAA wa R&B, Ed Sheeran yamemkuta! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya familia ya aliyekuwa mkali wa muziki huo, marehemu Marvin Gaye kutaka ilipwe dola milioni 100 (zaidi ya bilioni 225 za Kibongo) kwa kosa la kuibiwa wimbo.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Structured Asset Sales, inamdai Ed kiasi hicho cha pesa kutokana na kuiba Wimbo wa Let’s Get It On na kuubadili baadhi ya vitu kisha kuuita Thinking Out Loud. Ed anadaiwa kukopi midundo, melodi, sauti pamoja na kiitikio cha mbali kutoka katika wimbo huo uliowahi kuimbwa mwaka 1973.

Mtoto wa Marvin Gaye, Ed Townsend Jr kwa kushirikiana na Structured wameshafikia pazuri ambapo wamewalalamikia makampuni ya Sony/ATV Music, Atlantic Records na mwandishi ambaye ni Ed.Hata hivyo, bado Ed hajatoa ufafanuzi wowote juu ya madai hayo ya kuiba wimbo.

Wimbo wa Thinking Out Loud wa Ed uliachiwa Novemba, 2014 na kuwa namba moja katika chati kubwa duniani za Billboard.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad