Mahakama Yatengua na Kufuta Amri ya Kumkamata na Kumfunga Babu Tale

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama Yatengua na Kufuta Amri ya Kumkamata na Kumfunga Babu Tale
Mahakama Kuu imetengua na kufuta amri ya kuwakamata na kuwafunga gerezani wakurugenzi wa Tip Top Connection Company Limited, Hamis Shaban Taletale maarufu Babu Tale na ndugu yake Idd.

Uamuzi wa kufuta amri hiyo ulitolewa juzi na Jaji Edson Mkasimongwa baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa halali kutokana na mamlaka iliyoitoa kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Februari 16 naibu msajili wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri aliamuru Babu Tale na nduguye Idd wakamatwe na kupelekwa kifungoni katika Gereza la Ukonga kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama na Aprili 4 alitoa na kusaini hati ya kuwakamata.

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016 ndugu hao waliamriwa kumlipa fidia ya Sh250 milioni, mhadhiri wa dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kutokana na makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad