Serikali Yatengua Katazo la Wananchi Kuzuiwa Kupanda Meli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye ametengua katazo la wananchi kuzuiwa kupanda meli ya serikali hadi wawe na vitambulisho vya uraia au cha mpiga kura jijini Mwanza.

Nditiye amesema kuwa utaratibu wa awali uendelee kutumika hadi pale watakapo kaa upya kujadili ni njia ipi sahihi itakayoweza kuwawezesha wananchi kupata huduma ya usafiri bila kikwazo.

Nditiye ameongeza kuwa suala hilo lilitokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina ya Shirika la Meli pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama jijini humo.

“Wananchi wanamatatizo mengi, unapoanza kumchanganya na mambo ya vitambulisho tena unakuwa unawavuruga naomba utaratibu wa awali utumike na tuangalie utaratibu mwingine hapo baadaye”, amesema Nditiye.

Mamia ya abiria waliotakiwa kusafiri kwa meli ya Mv.Nyehunge kutoka jijini Mwanza kuelekea wilayani Ukerewe wamekwama kwa siku nne katika bandari ya Mwaloni Kirumba jijini humo baada ya kushindwa kutekeleza sharti linalomtaka kila msafiri kuwa na kitambulisho rasmi cha uraia au kupigia kura.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad