Barakah The Prince: Baada Ya Kusoma Biblia na Quran Nimeamua Kuwa Muislam Ili Kuwa Karibu na Mungu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Barakah The Prince: Baada Ya Kusoma Biblia na Quran Nimeamua Kuwa Muislam Ili Kuwa Karibu na Mungu
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefungukia uamuzi wake wa kubadilisha dini kutoka kuwa mkristo na sasa kuamua kuwa Muislamu.

Barakah amedai kuwa maamuzi hayo ya kubadilisha dini hawakuwa ya ghafla bali yalichukua  muda mrefu hadi kuyatekeleza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, amesema kuwa amejitahidi kusoma Biblia na Quran na akaja kubaini kuwa Uislamu ndio dini yake pekee kwa sasa ambayo itamuweka karibu na Mungu.

Baada ya kusoma biblia sana na kusoma Quran sana kukawa kuna vitu nikawa nimeipenda dini ya kiislamu Lakini pia naamini Mungu ni mmoja na tunamuamini Mungu mmoja tofauti ni dini tu”.

Lakini pia Barakah ameweka wazi kuwa pamoja na kubadilisha dini na kuwa Muislamu na kuupenda zaidi Uislamu lakini bado anasoma biblia kwani anataka kumjua Mungu zaidi na kuwa karibu naye.

Siku za nyuma baada ya Barakah kubadilisha dini na kuwa muislamu kuna tetesi zilidai kuwa alibadili dini kwa ajili ya mpenzi wake Naj ambaye ni Muislam taarifa ambazo Barakah alizikataa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad