Baba Atiwa Mbaroni kwa Kumpa Mimba Mwanaye wa Kumzaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba Atiwa Mbaroni kwa Kumpa Mimba Mwanaye wa Kumzaa
Jeshi la Polisi limemfikisha mahamani mwanaume mmjoa, Jacob Shabani (30) mkazi wa Kijiji cha Wanzamiso, Kata ya Igokelo wilayani Misungwi mkoani wa Mwanza, kwa tuhuma ya kufanya mapenzi mara tatu na mwanaye wa kumzaa na kumpa ujauzito.



Akisomewa hati ya mashtaka jana Septemba 25, 2018 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Erick Marley, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Ramsoney Salehe amedai tangu 2015 mshtakiwa alikuwa akiishi kinyumba na mwanaye mwenye umri wa miaka 17.



Imedaiwa kuwa huyo alipata ujauzito na mimba ikaharibika na mwaka 2016 akapata mimba ya pili na kujifungua mtoto wa kike ambaye alifariki mwaka huo huo na sasa amejifungua mtoto ana wiki mbili na ana ubini wa baba.



Amesema wamebaini jambo hilo kwa kuwa katika kadi hiyo, jina la baba linasomeka, Jacob Shabani ambapo Salehe ameiileza mahakama kuwa upelelezi umekamilika na shauri hilo kinaweza kusikilizwa na kuna mashahidi wanne na kielelezo cha kadi ya kliniki.



Hakimu Marley ameahirisha kesi hiyo ya jinai namba 74 ya mwaka 2018 hadi Oktoba 2, 2018 na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kwa kukosa mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh1milioni.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad