Bondia Aliyetakiwa na Hassan Mwakinyo Mmshauri Hili, Anthony Joshua Kabla ya Kuingia Ulingoni Hapo Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bondia Aliyetakiwa na Hassan Mwakinyo Mmshauri Hili,Anthony Joshua Kabla ya Kuingia Ulingoni Hapo Kesho
Bondia aliyetajwa na Mtanzania, Hassan Mwakinyo kuwa ndiyo tageti yake katika mapambano yajayo, Amir Khan amemshauri bingwa wa Dunia wa IBF, WBA na WBO, Anthony Joshua kuhakikisha mapambano yake anafanyia Marekani ili kuwa nyota wa ulimwengu mzima.

Khan amesema kuwa yeye kwa hivi sasa anafahamika ulimwengu mzima kwa sababu ya mafanikio aliyopata katika mapambano yake ya Marekani, wakati bingwa huyo wazamani wa dunia uzito wa light-welterweight akiwa amepambana zaidi ya mapambano 10 huko Las Vegas na New York Madison Square Garden.

Mwanamasumbwi huyo amesema King Joshua ambaye anatarajia kushuka ulingoni hapo kesho siku ya Jumamosi kutetea mkanda wake dhidi ya Alexander Povetkin kwenye uwanja wa Wembley ulimwengu mzima ungemfahamu kama angezipiga Mmarekani na kuachana na tamaduni za kupigana mapambano yake England.

“Ndiyo, kama unahitaji kuwa nyota wa ulimwengu mzima ni lazima uwende ukapigane Marekani, ndoto zangu ilikuwa kupigana Las Vegas, Madison Square Garden maeneo ambayo Muhammad Ali na Mike Tyson wamepata kupigana,” amesema Khan.

Khan ameongeza “Kivyovyote vile litakavyo onekana Marekani basi huonekana dunia nzima, nilianza kuwa na jina kubwa baada ya kupambana Marekani.”

“Watu wa Pakistan walianza kunifahamu, wakati nilipo pigana pambano langu la kwanza England hakuna aliyenijua Pakistan lakini wao na India walianza kunifahamu baada ya pambano langu kufanyika Marekani ukweli ni kuwa ukipambana Marekani hukufanya wewe kuwa maarufu ulimwenguni.”

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye anatarajia kupambana na mkongwe, Manny Pacquiao Desemba 8 mwaka huu anaimani kuwa Joshua angetengeneza mkwanja mrefu zaidi kama pambano lake lingefanyika nchini Marekani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad