BREAKING NEWS: Msafara wa Rais Magufuli wapata ajali Mara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BREAKING NEWS: Msafara wa Rais Magufuli wapata ajali Mara
Msafara wa Rais Dkt. John Magufuli uliokuwa ukielekea wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, umepata ajali katika Kijiji cha Kasuguti, kata ya Kisorya, wilayani Bunda mkoani Mara, leo Septemba 4, 2018 baada ya magari manne kugongana katika eneo ambalo barabara ilikuwa ikijengwa.

Taarifa za awali zinadai kuwa, waandishi wawili wa habari wamejeruhiwa baada ya gari walimokuwa kupinduka.

Kwa mujibu wa Mkuu Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mara, R.T.O Steven akizungumza na Global TV Online, amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kusema kuwa miongoni mwa gari zilizopata ajali moja ni waandishi wa habari na nyingine ni ya TAKUKURU.



Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni vumbi lilikuwa limetapakaa barabarani kutokana na msafara huo hivyo madereva kushindwa kuona vizuri njia lakini hakuna madhara makubwa licha ya gari moja kubondeka ubavuni baada ya kupinduka.

Ameongeza kuwa, magari yote yameshafika eneo la ambalo Rais Magufuli amekwenda kufanya ziara wala hakuna taarifa ya mtu aliyepelekwa hospitali kwa kuumia.

Taarifa nyingine kutoka eneo la tukio zinadai kwamba gari lingine lililopata ajali ni la Chama Cha Mapinduzi mkoa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad