Harmonize Bado Ananipenda Sema ni Pepo tu- Wolper

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Harmonize Bado Ananipenda Sema ni Pepo tu- Wolper
MSANII wa filamu nchini na mjasiriamali, Jacquiline Wolper amesema katika historia yake ya mahusiano kila mwanamume anayeachana naye anakuwa bado anamuhitaji licha ya yeye kuwakacha na kutohitaji mawasiliano nao wala kusogeleana.



Woler amesema hayo usiku wa kuamkia leo  kwenye ukumbi wa King Solomoni wakati akihojiwa na wanahabari kuhusu kukataa kukimbia salam ya Harmonize hivi karibuni kwenye moja ya event.



“Ujue mimi kila nikiachana na mwanaume anakuwa bado ananipenda, pale nilikimbia kwa sababu nikiachana na boyfriend, huwa sipendi niendelee kuwasiliana naye wala kusogeleana naye, sipendi kusalimiana na X.



“Ilishawahi kutokea X ananihitaji kwa ajili ya mambo ya kibiashara lakini kwa sababu nakuwa sihitaji kabisa kuwasiliana nao nili-crash halafu nikakosa dili, hilo ni pepo ambalo ninalo nadhani nitamwambia mchungaji aniombee,” alisema Wolper.



Akizungumzia sakata la kukacha ujaji wa Miss Lake Zone, Wolper amesema taji hilo limeshapoteza mvuto ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hivyo walitumia jina lake ili kuwavuta watu japo ilibuma.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad