Makonda Afunguka Kuhusu Mgambo Aliyemshambulia Mwananchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Afunguka Kuhusu Mgambo Aliyemshambulia Mwananchi
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ameagiza mgambo waliopiga raia katika eneo la Bunju mkoani humo kuchukuliwa hatua kali kwani walichokifanya haukuwa mpango wa mkoa.


Akiongea leo jioni makonda amekemea vikali kitedno hicho amabacho kimefanyika kwenye ofisi ya mtandaji wa kata ya Bunju ambapo mgambo hao wamepiga raia na kuwajeruhi akiwemo mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju kutokana na kushindwa kulipa Sh. 50,000 ya taka.

''Nimeshtuka sana baada ya kuona video hiyo sio kitendo cha kufanywa na watendaji kwani lengo letu ni kusimamia usafi na si kupiga raia, nalaani kitendo hicho na naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi yao'', amesema.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limethibitisha kuwashikilia mgambo watatu wa manispaa hiyo ambao wamehusika katika tukio hilo na taratibu za kisheria zinaendelea na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Murilo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Goodluck Festo, Rehema Nyange na Kelvin Edson, ambao wote ni mgambo wa manispaa hiyo huku akibainisha kuwa mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Siku za hivi karibuni zimesambaa picha za video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mgambo wakitoa kipigo kwa watu na kuzua taharuki, wengi wakiwa ni wafanyabiashara ndogondogo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad