Huyu Ndie Mchungaji Aliyepigwa Risasi 40 na Majambazi Bila Kupenya Mwilini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Huyu ndie Mchungaji aliyepigwa risasi 40 na majambazi bila kupenya mwilini
Wakati ulimwengu ukibuni njia ya kuweza kubuni mavazi ambayo yatazuia risasi kutokupenya kiurahisi kwenye mwili wa binadamu, hii ni tofauti kwa Mchungaji wa Kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International, David Elijah kutoka Nigeria ambaye wiki iliyopita amenusurika kifo kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani.

Mchungaji David siku ya Ijumaa Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria alikuwa anaenda kanisani kwake akiwa kwenye gari alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi.

Gari hilo lilitobolewa karibia lote kwa risasi lakini mpaka maaskari wanafika eneo la tukio, walimkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo.

Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo.

Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo siku ya Jumamosi baada ya kujiridhisha kuwa mtu huyo alikuwa salama na ni raia mwema.

Mchungaji David anatajwa kuwa moja ya wachungaji vijana wenye utajiri Mkubwa nchini Nigeria. Baada ya tukio hilo la kushambuliwa jana David alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika maburungutu ya fedha huku akiweka Captions kuwa yupo nchini Malaysia kikazi.

Maoni mengi ya wadau mitandaoni nchini Nigeria yanaonekana kushangazwa na tukio hilo, huku wengi wao wakidai kuwa Mchungaji huyo anatumia nguvu za giza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad