Khadija Kopa Afunguka Kuhusu Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Khadija Kopa Afunguka Kuhusu Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya
Mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Khadija Omar Koppa, amewakingia kifua wanandoa wawili kutoka tasnia ya sanaa ya bongo, Irene Uwoya na Dogo Janja, na kusema kwamba wawili hao wanastahili kuwa pamoja.


Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Khadija Kopa amesema kitendo cha watu kumuona Dogo Janja ni mdogo kwa Irene Uwoya si kweli, kwani hata Irene Uwoya ni mdogo isipokuwa ana mwili mkubwa.

“Mbona nyie Irene na Dogo Janja mnawaonea sana!? Hivi yule Irene nyie mnamuona mkubwa sana kwa sababu ya ule mwili!? Wala si mkubwa yule mtoto mdogo yule wa juzi, yule Dogo Janja kimwili chake kidogo dogo, ndio kampita lakini sio wa hivyo, lakini vilevile yule si mdogo, mdogo kwa mama yake ndio mwenye kujua kadi yake ya clinic iko wapi, na alokuwa anampeleka kupiga sindano, kwa Irene sio mdogo yule, yule mtu mzima kashaacha shule na mambo yake yapo kama kawaida”, amesema Khadija Kopa.

Khadija Kopa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Dogo Janja kumuoa Irene Uwoya sio ajabu kwani hata Mtume Mohamad kwenye imani ya dini ya Kiislam, alioa mwanamke aliyemzidi umri.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad