Inasikitisha Mama Amchoma Moto Mwanaye wa Miaka 2 Kisa Kuchezea Sehemu Zake za Siri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Inasikitisha Mama Amchoma Moto Mwanaye wa Miaka 2 Kisa Kuchezea Sehemu Zake za Siri
Mtoto mwenye umri wa miaka 2 na miezi 8 achomwa moto na mama yake mzazi kwa kushirikiana na bibi wa mtoto huo kwa madai ya kujichezea sehemu zake za siri.

Akionesha kukasirishwa na ukatili huo Baba mzazi wa mtoto huyo Ali Khamis Mbarouk maarufu Ali Gaga mkazi wa Koani amesema kitendo hicho kimefanyika mtaa wa Kwahani wilaya ya Mjini Unguja ambapo Mama mzazi na Bibi walimchoma moto wa makaratasi kwenye vidole vya mikono ya mtoto huyo na hadi sasa hali yake sio nzuri.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho mama mzazi wa mtoto ambaye alikuwa mke wake alimpigia simu majira ya usiku  baada ya kuona hali ya mtoto sio nzuri kutokana na kulia sana hali iliyopelekea kupatwa na homa.

“Asubuhi nilikwenda kumuona mtoto wangu na kumkuta katika hali mbaya anaumwa na hawezi kushika kitu chochote hivyo nikampeleka hospitali na madaktari baada ya kuona hali ya mtoto walilaani kwani adhabu zipo nyingi kwanini wamchome moto” Amesema baba mzazi wa mtoto.

Nae Sheha wa shehiya ya Kwahani Machano Mwadini Omar amelaani kitendo hicho na kusema si kitendo kizuri wao kama wazazi kumtendea mtoto wao hivyo ameviomba vyombo vya sheria vichukuwe hatua iwe fundisho ili tukio kama hilo lisije kujirejea.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad