Matokeo ya Mchezo wa Simba na Yanga Haya Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya presha ya game ya watani wa jadi ya Simba na Yanga kutawala kwa zaidi ya wiki moja na nusu sasa, Jumapili ya September 30 2018 ndio siku ambayo ubishi ulimalizika kwa timu hizo kukutana uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo mashabiki wa timu zote wakiwa wamejitokeza kwa wingi.

Game ya leo Simba  walifanikiwa kuutawala mchezo na kupata nafasi nyingi zaidi ya Yanga, kitu ambacho kilizidisha furaha kwa mashabikiwa Simba wakiamini timu yao itaondoka na point zote tatu lakini licha ya kupata nafasi zaidi ya sita, Yanga walifanikiwa kuidhibiti Simba na kuufanya mchezo umalizike kwa sare tasa 0-0.

Hii ndio mara ya kwanza kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na kocha wa Simba Patrick Aussems kuziongoza timu hizo katika mchezo wa watani wa jadi (Kariakoo Derby), sare hiyo sasa inaifanya Yanga kutimiza jumla ya point 13 katika msimamo wa Ligi wakati Simba wanafikisha jumla ya point 11.

Kwa upande wa takwimu za mchezo huo Simba walipiga mashuti 10 yaliolenga lango wakati Yanga matatu,  Simba walipiga jumla ya kona 11 Yanga wao wakiishia kona moja pekee, Yanga wamecheza madhambi mara 27 Simba mara 12 mwisho Simba waliufanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 62 kwa 38 dhidi ya Yanga kwa dakika zote 90.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad