Mhandisi kivuko cha Mv Nyerere chini ya ulinzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mhandisi kivuko cha Mv Nyerere chini ya ulinzi
Mhandisi wa kivuko cha Mv Nyerere, Agostino Charahani  aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza yupo chini ya ulinzi, MCL Digital imeelezwa leo Alhamisi Septemba 27, 2018.

Mmoja kati ya madaktari wanaomhudumia mhandisi huyo kwa sharti la kutotajwa jina ameieleza MCL Digital kuwa mhandisi huyo analindwa.

Charahani aliokolewa akiwa hai, ikiwa ni baada ya kupita  saa 48 tangu kivuko hicho kupinduka Machi 20, 2018.

"Hapa watu hawajui kwamba maofisa wa usalama wapo wanazunguka humu. Inakuwa vigumu kuwabaini maana wamevalia kiraia," amesema daktari huyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa mhandisi huyo anashikiliwa kutokana na sababu kubwa mbili ambazo ni kumuepusha na wananchi wenye uchungu wa kupoteza ndugu katika ajali hiyo na kutoa ushahidi jinsi kivuko kilivyopinduka.

"Hapa huwezi kutoa hukumu ya moja kwa moja kuhusiana na mhandisi huyo kupewa ulinzi wanaomshikilia wanajua na wana sababu zao,” kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, ofisa habari na mahusiano wa Bugando,  Lucy Mogele alipoulizwa kuhusu mhandisi huyo alikataa kuzungumza.

Kivuko cha Mv Nyerere kimenyanyuliwa leo ikiwa ni siku ya saba tangu kilipopinduka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 228.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad