Moto wateketeza soko la Mlango Mmoja Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Moto wateketeza soko la Mlango Mmoja Mwanza
Moto usiojulikana chanzo chake umeteketeza soko la Mlango Mmoja jijini Mwanza leo alfajiri Septemba 28,2018.

Jitihada za kudhibiti moto huohuo unaoteketeza mabanda ya wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa eneo hilo zinaendelea.

Magari ya zimamoto na uokoaji yanaendelea kuuzima moto huo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana ambaye yupo eneo la tukio amesema mpaka inafikia saa mbili asubuhi walikuwa wamezima moto huo kwa asilimia 90.

Katika kuhakikisha usalama unakuwapo eneo hilo, Kamanda Shana amewaonya vijana na watu wengine wenye nia ya kuiba mali ya watu zilizosalia, kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali.

"Niwahakikishie kwamba hapa usalama umeimarishwa na yeyote atakayejaribu kuleta ujuaji hapa, asimlaumu mtu," amesema Kamanda Shana huku akisema chanzo cha moto huo hakijajulikana

Mmoja kati ya wafanyabiashara wa soko hilo, Elias Wambura amesema huenda moto huo ukawa umesababishwa na mamalishe ambao wana tabia ya kuacha majiko yao yakiwa na moto kwa lengo la kuyakuta alfajiri na kuendelea na shughuli yao ya mapishi.

"Sina uhakika lakini kwa upande wa hao wa mama, wana tabia ya kufunika moto kwenye majiko ili wakija asubuhi, isiwape taabu kuuwasha," amesema Wambura.

Mwenyekiti wa masoko jijini Mwanza, Hamad Nchora amewapongeza wafanyabiashara wa soko la Mlango Mmoja kwa ushirikiano walio nao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad