Vichambo vya Instagram Vyamfikia Muandaaji wa Miss Tanzania Anena Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mratibu wa shindano la Miss Tanzania na Mkurugenzi wa The Look Company, Bi. Basila Mwanukuzi amesema alitegemea kuona baadhi ya watu kupinga zawadi aliyopatiwa mshindi wa taji la Miss 2018, kwa madai walinyimwa vibali vya kuyaendesha hivyo wameibukia katika ukosoaji na sio kujenga.


Bi. Mwanukuzi ametoa kauli hiyo leo Septemba 10, 2018 alipokuwa anazungumzana www.eatv.tv baada ya kupita siku moja tokea kumalizika kwa shindano hilo kumalizika na kuibuka mjadala mzito mitandaoni, kuwa zawadi ya gari aliyopatiwa mshindi aliyetwaa taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune haifanani na hadhi na thamani aliyokuwa nayo.

"Miss Tanzania anaposhinda zawadi kubwa anayoipata ni kuwakilisha nchi na hivyo vingine ni zawadi za nyongeza tu. Hivyo napinga suala hilo kuwa hii zawadi haina thamani, najua hizi ni vita tu vya mitandaoni na watu wanavyopotosha lakini huwezi kuwazuia. Pia hao wanaosema hayo maneno tunapaswa kujiuliza wao wamechangia kitu gani maana wanatarajia mshindi apatiwe zawadi kubwa wakati wao wenyewe hakuna walichokitoa.....

Unatakiwa ukosoe pale ulipoweza kuchangia hata senti tano, hivi vitu vyote nimenunua mwenyewe kwa pesa yangu kutokana na mapenzi niliyokuwa nayo kwa wadogo zangu. Hiyo zawadi watu wanazungumzia mitandaoni lakini waliokuja kwenye sherehe yenyewe waliiona vizuri tu. Gari ina thamani ya milioni 15 na hakuna 'limit' ya zawadi iliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za mashindano", amesema Mwanukuzi.



Miss Tanzania  Queen Elizabeth Makune (kushoto) akivalishwa taji la Miss Tanzania na aliyekuwa anashikilia taji hilo Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumai.

Mbali na hilo, Mwanukuzi amesema kitu kikubwa alichoweza kukifanyia marekebisho katika mashindano hayo ni kuwawezesha washindi wote wa 'Top five' kuwa na mikataba ya kutangaza utalii unaopatikana nchini Tanzania jambo ambalo lilikuwa halifanyiki katika mashindano yaliyopita.

Bi. Basila Mwanukuzi ambaye alikuwa Miss Tanzania mnamo mwaka 1998, haya ndio mashindano yake ya kwanza kuyaendesha tokea alipoyachukua rasmi kutoka kwa kwa muandaaji Hashim Lundenga mwanzoni mwaka huu ambaye alitolewa katika uendeshaji huo kwa kile kinachodaiwa kuwepo ubabaishaji na uhuni katika tasnia hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad