Auawa akidaiwa kuoa mke wa pili bila kushirikisha familia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Auawa akidaiwa kuoa mke wa pili bila kushirikisha familia
Mkazi wa Kijiji cha Isongole wilayani Ileje mkoani Songwe, Joseph Chomo (55) ameuawa kwa kupigwa na mkewe pamoja na watoto akidaiwa kuoa mke wa pili bila kuwashirikisha.

Akizungumza na Mwananchi jana, mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude alisema tukio hilo lilitokea saa sita usiku wa kuamkia jana huku akibainisha kwamba chanzo halisi kinaendelea kuchunguzwa ili kubaini ukweli.

Mkude alisema hadi jana mke na watoto wawili wa Chomo walikuwa wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea.

Akizungumzia mkasa huo, Elifa Kalago alisema usiku huo walisikia sauti ya Chomo akiomba msaada na walipofika nyumbani kwake walimkuta amelala mlangoni huku akitokwa damu nyingi.

Alisema alipoingia ndani aliwakuta mke na watoto wawili wakisafisha damu iliyokuwa imetapakaa katika nyumba yao.

Kalago alisema baada ya kuwauliza sababu ya tukio hilo hawakutoa jibu, ndipo walipoamua kumpeleka Chomo hospitali, lakini alipoteza maisha wakiwa njiani.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Ikomba Kayuni alisema wanafamilia hao walikuwa na ugomvi wa siku nyingi na ulianza baada ya baba mwenye nyumba kuoa mke wa pili bila kuwashirikisha, japokuwa awali ugomvi huo ulionekana kwisha.

Hilo ni tukio la pili katika kipindi cha wiki mbili mkoani Songwe, ambapo mwishoni mwa mwezi uliopita mkazi wa Kijiji cha Bupigu wilayani Ileje alifariki dunia baada ya kupigwa na mkewe kutokana na wivu wa mapenzi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad