Kauli ya Meya wa Ubungo Kuhusu Kuhamia CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Meya wa Ubungo (CHADEMA), Jacob Boniface.

Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Boniface Jacob amesema kuwa hayuko tayari kuhama wanaozusha waache kuota ndoto zisizo wezekana.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa 'twitter' Jacob ameandika kuwa hayuko tayari kufanya hivyo na yuko tayari kukipigania chama chake hadi kifo chake.

"Waambieni wanaotamani nihamie CCM, nipo tayari kufa nikipigania chama changu CHADEMA na Sipo tayari kuwa takataka kwa kuhamia CCM!, iwe kwa pesa vitisho au kifo acheni kuota ndoto zisizowezekana", amesema Jacob.

Oktoba 6, katika mahojiano yake na  www.eatv.tv Meya Jacob alisema kuwa katika vitu ambavyo hatamani kuvisikia kwa mtu yeyote ni kwamba yeye binafsi ana  mipango ya kuhamia CCM na kusema kauli hiyo ni inalenga kumdhalilisha.

“Unajua wananchi wanapaswa kujua kuwa vyama vya upinzani huwa vinapata tabu sana kwenye uchaguzi hapa nchini lakini niwaambie hatutakata tamaa, tutaendelea kutetea haki zetu", amesema Jacob.

Meya wa Ubungo amekuwa miongoni wa viongozi wa mwanzo kutajwa kuwa wako mbioni kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla ya kushamiri kwa hamahama ya viongozi wa upinzani wanaojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad