Rais wa TLS Ampongeza Waziri Lugola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa TLS Ampongeza Waziri Lugola
Rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (TLS), Fatma Karume amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kwa agizo alilotoa kwa Jeshi la Polisi, kutoa dhamana kwa watuhumiwa siku zote saba za wiki kwa masaa 24.


Karume ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha  East Africa BreakFast kinachoruka East Africa Radio kuanzia saa 11 Alfajiri, ambapo amesema suala la Polisi kutoa dhamana Jumamosi na Jumapili ni wajibu wao, kama wanafanya kazi siku hizo na wanalipwa

Karume ameongeza kuwa Polisi wana wajibu wa kuwapa watu dhamana, na iwapo watalazimika kuendelea kumshikilia mtuhumiwa wanatakiwa kuongeza masaa 8, na iwapo itahitajika zaidi ni lazima wapate kibali cha mahakama.

Rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (TLS), Fatma Karume.

"Polisi sio mahabusu, mahabusu ni jela na huwa pale mahakama imeamua kuwa wewe hustahili kupata dhamana, polisi hakuna mahabusu, polisi hawana haki ya kukuweka selo kwa zaidi ya saa 24", amesema Karume.

Karume mesisitiza kuwa, "Inawezekana huyu mtu ana watoto, anafanya kazi na anatakiwa kazini, iwapo utamshikilia mtu na umemnyima haki ya dhamana, akakaa bila kwenda kazini labda, ikamuathiri kufukuzwa kazi, ni umemnyima haki yake".

Septemba 30, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Nchini kuhakikisha dhamana kwa watuhumiwa inatolewa kwa saa 24 katika siku zote 7 za wiki, tofauti na zamani ambapo ilikuwa inatoka mwisho Ijumaa jioni.

Lugola alitoa agizo hilo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad