Breaking: Necta Yafuta Matokeo ya Mitihani ya Dalasa la Saba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Breaking: Necta Yafuta Matokeo ya Mitihani ya Dalasa la Saba

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha-kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.

Miongoni mwa shule zilizokumbana na kadhia hiyo ya kufutwa kwa matokeo hayo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopoHalmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji, Shule za Msingi za halmashauri ya Chemba ambao viongozi wake walitajwa kuhusika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo. Amesema Charles Msonde.

Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad