Rashid Matumla Kupanda Ulingoni Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rashid Matumla Kupanda Ulingoni Leo
Mwana masumbwi wa zamani nchini Tanzania ambaye aliwahi kushinda mkanda wa WBC, Rashid Matumla anatarajia kupanda ulingoni hii leo kuzichapa na Matibwa Ally, pambano litakalopigwa katika uwanja wa ndani wa taifa.


Matumla atashuka ulingoni hii leo katika pambano kwaajili ya kuchangia watoto yatima kupata bima za afya pamoja na kuchangia damu salama kwaajili ya wamama wajawazito.

“Kuanzia saa tano na nusu milango itakuwa wazi kwaajili ya watanzania kuingia, tunawaomba wachangie watanzania wenzao. Na sisi kama ‘maboxer’ tuna kauli mbiu inasema ‘Toa damu salama ili uokoe maisha ya wamama wajawazito, lakini pia mchangie mtoto yatima, leo ni wa mwenzio kesho ni wako’ ”, amesema Said Omari ambaye ni Mratibu wa tamasha hilo.

Kwa upande wake, Rashid Matumla amewataka mashabiki wa ndondi wajae kwa wingi uwanjani waje washuhudie wakongwe namna walivyokuwa wakipigana mapambano yao na kushinda hapo zamani.

Matumla alistaafu mchezo wa ndondi akiwa amepigana mapambano 58 , akishinda mapambano 41, akipoteza mapambano 15 na mapambano mawili yakiisha bila ya kupatikana mshindi. Pambano lake la mwisho ni la mwaka 2012 alipopambana na Mjerumani, Benjamini Simon na kupigwa kwa ‘KO’.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad