Zari Adaiwa Kutafuta Mwanasheria Wa Kumshughulikia Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amedaiwa kutafuta mwanasheria kwa ajili ya kumsimamia mzazi mwenzake.

Tangu Diamond na Zari walipoachana mapema mwaka huu wamekuwa wakijaribu kutafuta njia bora ya kulea watoto wao wawili wadogo na mara kwa mara Zari amemtuhumu kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kama Baba.

Global Publishers wanaripoti kuwa Zari mwanasheria kwa ajili ya kumsimamia Diamond ili awalee watoto wake katika misingi bora licha ya kuwa wameshatengana.

Chanzo cha karibu cha Familia hiyo kimeiambia gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa Zari ni mwanamke ambaye yuko ‘siriaz’ na malezi ya watoto hivyo ameamua kumwekea mzazi mwenzake huyo mwanasheria ili aweze kuwajibika kwa asilimia mia moja bila kukosa hata jambo moja la msingi.

Unaambia siri ya Diamond kwenda Sauz (Afrika Kusini) kila mwezi ni baada ya kuwekewa mwanasheria huyo ambaye anamfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha haendi kinyume na matakwa ya sheria.

Unajua hata akiwa na shoo vipi ameambiwa ajipange ili kutofautiana na ratiba za watoto na akifika nyumbani pale kwa Zari wanalala chumba tofauti ingawa siku nyingine anakwenda kulala hotelini”.

Baada ya taarifa hizo GPL lilimsaka Diamond ambaye alifungukia tuhuma hizo na kusema:

Waswahili nimewazoea sana tu, wasiponiongelea na Zari hawaoni sawa, mimi huwa nakuja huku kwa ajili ya kuwaona watoto wangu, natimiza majukumu kama baba, hayo mengine nawaachia wao”.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad